Bismillahir Rahmaanir Rahiim
E.D.K. FUND
p.o.box 1648-
iringa-tanzania
edk.fund@gmail.com
REF NO. edkl01/11 DATE: 25/02/2011 - 23/03/1432 H
Ndugu Muislamu,
Assalam Alaikum Warahmatullah Wabarakatuh,
YAH: MFUKO WA ELIMU YA DINI YA KIISLAMU (EDK-FUND).
katika manispaa yetu ya Iringa kuna idadi ya Shule za Msingi arubaini (40) na Shule za Sekondari ishirini na mbili (22) katika jumla ya kata kumi (10).
Ongezeko kubwa la shule za kata, limetoa nafasi kwa ongezeko la wanafunzi wanaochaguliwa kujiunga na elimu ya sekondari, kwa mara ya kwanza katika historia ya nchi hii, vijana wengi wa kiislamu wamepata nafasi ya kuendelea na masomo ya sekondari kinyume na ilivyokuwa huko nyuma.
Katika utafiti usio rasmi uliofanywa na kamati ya EDK katika shule zote za msingi na sekondari zilizopo katika Manispaa ya Iringa, iligundulika kuwa asilimia 100 ya shule zote zina vipindi vya dini ya kiislamu na kikristo katika ratiba zake, na asilimia 99.5% ya vipindi vya dini ya Kikristo vinasomeshwa kwa ngazi ya Msingi na Sekondari, na asilimia 90% ya vipindi vya dini ya Kiislamu havisomeshwi kwa kutokuwepo waalimu wa dini.
Kutokana na hali hiyo ya kusikitisha, baadhi ya wanafunzi wa kiislamu wamejikuta wanalazimika kuingia katika vipindi vya kikristo kwa ajili ya kuongeza alama zao katika mitihani, katika mazingira kama hayo, wanafunzi watano wa kiislamu wameritadi katika shule tofauti hapa Manispaa mwaka 2010.
Hali hii, ilitufanya baadhi yetu tukae na kutafakari nini cha kufanya kuokoa kizazi hiki cha kiislamu? ! . baada ya Shuura ya pamoja, tulifikia maazimio yafuatayo:
1. Iandaliwe program maalumu ya Elimu ya Dini ya Kiislamu (EDK) Mashuleni itakayosimamiwa na kamati anzilishi ya mpango huu.
2. Mpango mkakati wa program uwe ni kupata waalimu wa somo la dini ya kiislamu kwa kila shule (Msingi na sekondari) iliyopo katika manispaa ya Iringa kwa kutumia rasilimali watu zilizopo.
3. Ili program hii iweze kufanikiwa na kuwa endelevu, ilionekana kuwa ni lazima iwezeshwe na nyenzo saidizi kama:
a. Nauli za waalimu watakaokwenda kusomesha shule hizo.
b. Vitabu vya kusomeshea na mitaala yake.
c. Semina za mafunzo (capacity building) kwa waalimu watakaojitolea.
d. Usafiri wa Baiskeli kwa ajili ya shule zilizopo maeneo yasiyofikika kirahisi.
e. Ofisi itakayotumika kusimamia program hii.
f. Seti moja ya Computer ( cpu,monitor,keyboard,printer,ups)
Mafanikio:
a. Waalimu wa shule za msingi 40 wamepatikana.
b. Waalimu wa shule za Sekondari 22 wamepatikana.
c. Nauli za waalimu wote wa shule za msingi na sekondari zimepatikana.
d. Vitabu vya kusomeshea na mitaala ya shule za msingi na sekondari vimepatikana kwa kila mwalimu.
e. Ofisi ya kusimamia program hii imepatikana.
f. Zoezi la kufungua akaunti maalumu kwa ajili ya program hii linaendelea vizuri.
Angalizo:
- Kwa kuwa program hii ni endelevu, waislamu wote wanaombwa kuchangia katika mfuko huu kwa kuwasilisha michango yao kupitia kwa yeyote miongoni kwa kamati ya maandalizi hapo chini.
Kamati ya Programu (EDK – FUND)
1. UST. ABDULRAHMAN BOBSETH M/KITI 0788027733
2. UST. ZUBERI ADINANI KATIBU 0714522122
3. UST. ABUBAKAR CHALAMILA MJUMBE 0787459030
4. UST. SHAMS ELMI MJUMBE. 0784448484
WABILLAHI TAWFIYQ
No comments:
Post a Comment